Rwanda: Hali ya Taifa

Juhudi za Kuleta Ustawi na Kuiweka Rwanda Inayoshamiri Kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki.

 

Wengi wetu tumesikia mengi kuhusu Rwanda. Nchi yenye vilima vingi. Nchi yenye miji nadhifu yenye kuhadaa juu ya ukweli wa mambo. Kuna mengi yanaendelea katika taifa hili la Afrika Mashariki. Tovuti hii itakuwezesha kufahamu mambo mengi yanayohusu tailfa la Rwanda ikiwemo fursa na matumaini ya baadaye.

 

Pakua IlaniWito

Muhtasari

Rwanda ni nchi mwanachama wa Jumuiya ya Afrika iliyozungukwa na nchi kavu, ambayo mandhari yake ya milima ya kijani yaliipatia jina la utani la “nchi ya vilima alfu moja”. Inapakana na Uganda, DRC, Burundi na Tanzania.

Wapo wanyarwanda wengi wasiojua chochote kuhusu hii histoia yetu fupi ndani ya miaka 127. Huenda hata wakaiona kama mzigo wa matukio yanayotofautiana kwenye historia yetu, alama za takwimu zisizo na uhusiano. Wageni, kila wanapopata hamu ya kutaka kuijua Rwanda katika kila awamu au katikati ya awamu hizi, huyachukulia kama matukio yaliyojitenga, kama picha ya haraka kwenye filamu.

Hali ya Jamhuri ya Rwanda kwa kiwango kikubwa sana ni dhaifu. Miaka ishirini na saba tangu uingie madarakani utawala wa kiimla wa RPF ya jenerali Kagame imeipeleka Rwanda kwenye mtanziko mkubwa wa hofu, wengi kukaa kimya kwa kulazimishwa, taifa zima kukata tamaa na kutokuwa na matumaini.

Rwanda Katika Tawala Mbalimbali

1894-1916

Awamu Ya Kwanza: Utawala Wa Kijerumani

Ujerumani wanaweka utawala juu ya utawala wa mfalme wa Rwanda. Milki ya Rwanda ikawa chini ya koloni la Ujerumani la Afrika Mashariki ambalo lilijumuisha na Tanganyika.

1916-1962

Awamu Ya Pili: Utawala Wa Kibelgiji

Kama wajerumani kabla yao, Wabelgiji walianzia kwenye hatua ya usimikaji wa utawala wao kwa uvamizi wa kijeshi, kuweka tabaka juu ya uongozi wa kifalme uliopo.

Rwanda Ya Sasa

Miaka ishirini na saba tangu uingie madarakani utawala wa kiimla wa RPF ya jenerali Kagame umeipeleka Rwanda kwenye mtanziko mkubwa wa hofu, wengi kukaa kimya kwa kulazimishwa, taifa zima kukata tamaa na kutokuwa na matumaini. Simanzi ya taifa imeongezeka sana na kujilimbikiza kwa sababu karne nyingi ziliacha simanzi ambayo imezidi kuwa mbaya zaidi kila mabadiliko ya utawala yajapo. Wanyarwanda wapo katika hali ya kudumu ya magomvi na uasi.

Malengo Yetu

Wakati tunatazama mbele ya muongo mmoja kwenye miaka ya 2030, 2050 na 2100, hizi ni baadhi ya changamoto zinazoikabili Rwanda, mawazo chanya ya kuzingatia katika mijadala baina ya wanyarwanda, jirani zetu na ulimwengu kwa ujumla.

Kulileta Taifa la Rwanda Pamoja

Rwanda imekuwa katika miongo ya kutawanyika na utengano. Ni wakati sasa wa kulileta taifa pamoja.

Ubunifu wa kijamii na kiuchumi

Kuimarisha ujuzi na ubunifu wa Wanyarwanda katika mapinduzi ya nne ya viwanda.

Kusema ukweli kwa ajili ya haki

Kutengeneza mazingira salama kwa ajili ya ukweli kusemwa kwa lengo la kufufua badala ya kudumaza.

Kutulia ndani ya Jumui ya Afrika Mashariki

Mazuri ya Wanyarwanda wa sasa yatajengwa na changamoto na fursa zilizomo kwenye ukanda huu.

Pakua Ilani Yetu

Ilani ya Kuleta Pamoja Ustawi na Kuiweka Rwanda Inayoshamairi Katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Pakua Ilani