Ifahamu Rwanda

Maarufu kama nchi ya vilima elfu moja, Rwanda ina mengi yakujifunza kwa wageni na Wanyarwanda wenyewe.

HISTORIA KWA UFUPI

Uvamizi wa wakoloni wa kijerumani wa karne ya 19 ulitokea kipindi ambacho ufalme ulikuwa ukipitia mabadiliko ya kitawala kama matokeo ya kugombania madaraka miongoni mwa koo za kifalme za watusi. Ijapokuwa kwa karne nyingi Rwanda imetawaliwa na wafalme watusi, kubadilika kwa vurugu za matukio ilielezwa na wanahistoria kama mapinduzi ya Rucunshu (1896) yalikuwa alama ya wakati muhimu ulioamua namna gani nguvu za kisiasa zingepatikana, kulindwa na kupotezwa katika karne huko mbeleni.

Kupitia muingiliano wa hadithi zisizo za kweli, mashirika ya kijeshi, mipangilio ya kijamii na kiuchumi, Rwanda ina jamii ya mpangilio wenye ufalme kamili juu kabisa na wengine wote chini yake. Siyo kila watawaliwa walikuwa na hadhi sawa mbele ya mtawala. Kwa ufupi ni kuwa, watwa walikuwa chini kabisa ya mfumo huo wa kijamii na kiuchumi huku wahutu wakifuatia na wingi wao na watusi kwa uchache wao wakiwa juu kabisa.