Wito Wa Dharura

Vilima vya Rwanda vimekuwa maeneo ya uhalifu kwa muda mrefu. Ni Muda sasa wa kubadilika.

Ni Lazima Kuanza Leo, Siyo Kesho.

Kwa muda mrefu vilima vya nchi ya Rwanda vimekuwa maeneo ya uhalifu. Damu ya kupita kiasi imemwagwa kwenye vilima hivi, mabonde, kona na pembe ya hii nchi vumilivu. Ardhi yetu imeharibiwa mno kwa matendo ya vibaraka wenye njaa na vurugu ambao wameigeuza Rwanda kuwa kaburi kubwa kupitiliza. Hakuna familia hata moja Rwanda, zikiwemo familia za vibaraka ambao wameiacha nchi yetu patupu wameepushwa na simanzi, huzuni na majonzi. Kupitia matendo yetu, tofauti zote na ukimya wetu tumechangia huu uwendawazimu, machafuko na kuharibikiwa huku ambako kumeharibu jamii ya Rwanda kizazi na kizazi.

Kukomesha utekaji nyara, vita na mauaji ya kimbari

Kwa sasa taasisi za kiusalama za Rwanda zimegawanyika.  Ni lazima ziwe rasmi, zisijihusishe na uhalifu, zifanye kazi kitaalamu.

Majadiliano Mapana: Majadiliano ya mkataba wa jamii itakavyoishi

Lazima tuwe wakweli baina yetu na tuuseme ukweli kwa wale walioko madarakani na kwetu sisi wenyewe.

Kuituliza nchi ya Rwanda ndani ya Jumui ya mataifa ya Afrika Mashariki

Mazuri ya Wanyarwanda wa sasa yatajengwa na changamoto na fursa zilizomo kwenye ukanda huu.

Kusema ukweli kwa ajili ya haki

Kutengeneza mazingira salama kwa ajili ya ukweli kusemwa kwa lengo la kufufua badala ya kudumaza.

Ubunifu wa kijamii na kiuchumi

Kuimarisha ujuzi na ubunifu wa Wanyarwanda katika mapinduzi ya nne ya viwanda.

Kulileta taifa pamoja

Rwanda imekuwa katika miongo ya kutawanyika na utengano. Ni wakati sasa wa kulileta taifa pamoja.

Iko Wapi Suluhu Ya Wanyawranda?

Yatupasa wanyarwanda kutoutafuta muujiza nje yetu sisi. Ni lazima tutazame ndani yetu. Hapo ndipo suluhishi lilipo, kwenye fikra na matendo yetu. Lazima kuukabili ukandamizaji unaotuzuia kutambua ya kuwa sisi sote ni sehemu ya mwili mmoja au familia moja iitwayo Rwanda. Pale eneo moja la mwili linapoumwa, mwili wote unajeruhiwa. Hii ni shughuli ya mioyo na fikra zetu. Kwa kutambua kuwa tu jamii inayoumwa, lazima tukatae na kugomea mizizi ya majonzi. Hatuhitaji fedha, watu kutoka nje au idhini ya wale watusababishiao huzuni ili kuweza kuponya vidonda vyetu na kutibu majeraha ya wenzetu.

Ni lazima na tutajikomboa wenyewe kutoka kwenye ukandamizaji. Tutalileta pamoja na kuliponya taifa letu. Tutajipa nguvu wenyewe kwa wenyewe ili kutengeneza taifa endelevu na thabiti ambalo watu wake, familia na jamii kwa ujumla hushamiri. Tutaunda upya taifa la Afrika Mashariki lenye usalama wa kutosha na lenye kufanikiwa. Ni lazima kuanza leo, siyo kesho.

Pakua Ilani Yetu

Ilani ya Kuleta Pamoja Ustawi na Kuiweka Rwanda Inayoshamairi Katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Pakua Ilani