Fahamu Utume Wetu

Kwa pamoja, Ishakwe na Taasisi Ya Ukweli ya Rwanda wana malengo yafuatayo;

Ishakwe -Rwanda Freedom Movement

Lengo letu ni kuhabarisha umma ukweli juu ya Rwanda na mapambano yetu ya kuibadilisha nchi yetu kuwa taifa huru, lenye umoja, lenye mafanikio, lenye amani ndani yake na majirani zake. Wimbo wentu ni mmoja tu, tunapenda kuona; Rwanda iliyo huru, yenye umoja na mafanikio.

 

Maadili Yetu

Tunataka kukuza utu wetu wa kijamii; kuwathamini Wanyarwanda wote bila ubaguzi; haki ya kuwakumbuka wahanga wote wa mauaji ya kimbari na uhalifu mwingine; utakatifu wa maisha; huruma; kuheshimu haki zote za kimsingi za binadamu; ushiriki sawa katika nyanja zote za maisha ya taifa; usawa wa fursa; kuheshimiana na kuvumiliana; kukuza masilahi ya Rwanda; na kusema ukweli.

Utume Wetu

Tunataka kufanya kazi na Wanyarwanda wote ili kushinda aina zote za udikteta baada ya historia ndefu na yenye kuhuzunisha, kwa kuhamasisha kuongea ukweli, kuwakumbuka wahasiriwa wote, tukifanya kila liwezekanalo mamo haya hayajirudii kamwe, na kuwa watetezi katika mapambano ya kujenga Rwanda huru, yenye umoja na ustawi.
.

Tume ya Ukweli ya Rwanda ni taasisi ya kiraia iliyoanzishwa mnamo 2016 kwa lengo la kuchunguza na kuandika ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu, uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi ya binadamu, na mauaji ya kimbari kutoka 1962 hadi sasa ambayo yalifanywa na serikali ya Rwanda na watendaji wa jimbo.

Tume hii (Rwanda Truth Commission) inalenga kuthibitisha ukweli wa matukio ya vurugu na ya kutisha ambayo yamejibainisha nchini Rwanda tangu uhuru wa kisiasa kutoka Ubelgiji mnamo 1962. Tume inachambua mazingira ya kihistoria, kisiasa, kiuchumi na kijiografia ambayo yalichangia kutokea kwa matukio hayo.

Katika kazi yake, Tume inataka kufanya kazi kwa karibu na waathiriwa, manusura na wadau wote katika jamii ya Rwanda ili kupata ukweli ambao utachangia kuungana, kupatanisha na kuponya jamii ya Rwanda. Ni imani na matumaini ya Tume kwamba jamii nzima kuambiana ukweli italeta mabadiliko yanayohitajika kijamii, kisiasa na kiuchumi ambayo yatazuia kutokea tena kwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu, uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi ya ubinadamu na mauaji ya kimbari katika Rwanda.
Kazi ya Tume imejikita katika utafiti, elimu, ufikiaji na utetezi katika maeneo muhimu ili kutokomeza hali ya kutokujali na kukuza uwajibikaji juu ya:

  • KHaki ya Jinai
  • Kumbukumbu
  • Marekebisho ya Taasisi
  • Vurugu za Kijinsia
  • Watoto na vijana

    .

  • Njia za uponyaji na upatanisho
  • Kinga na utatuzi wa migogoro
  • Kujenga jamii na mifumo ya kiaifa ya kutoa angalizo mapema
    taratibu za kikanda na kimataifa za haki ya mpito
  • Utawala wa Sheria, Demokrasia, Usalama na Maendeleo ya Binadamu

Pakua Ilani Yetu

Ilani ya Kuleta Pamoja Ustawi na Kuiweka Rwanda Inayoshamairi Katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Pakua Ilani