Suala la ukabila ni jambo nyeti ambalo nyerere aligusia katika hotuba nyingi alizowasilisha.

Nyerere alikemea suala la ukabila kila wakati alipopata nafasi ya kuzungumza na hakutaka kabisa kuwe na maswali kama wewe ni kabila gani? Ni katika hilo alifanikiwa kwa kiasi kikubwa, siyo kawaida nchini Tanzania kuulizana kuhusu masuala ya ukabila.

“Nilikutana na mama mmoja akaniambia alikua akifanya kazi jumuiya ya afrika mashariki, akasema sisi watu wa uganda tulikua tunajuana kwa makabila yetu , watu wa kenya walikua wakijuana kwa makabila yao, huyu mkikuyu, huyu mluhya. Akasema lakini sisi watanzania hatujui makabila ya watu. Nikamwambia mama ni wakati huo, sasa hivi watanzania wanataka kujua makabila yao, ya nini?, mnataka kutambika? Majirani zetu walikua wanaiga kutoka Tanzania, sasa bila haya na sisi tunataka kuulizana makabila?

Mwalimu Nyerere katika hotuba yake ya mkutano mkuu wa CCM 1995.